Tanzania
ina eneo mraba la hekta 94.3 milioni, ambazo hekta 22 milioni
(23%) zimetengwa kwa hifadhi(ikiwa ni eneo kubwa la rasilimali ya
ardhi kutengwa kuliko nchi nyingine yeyote Kusini mwa Sahara),
ikijumuisha Mbuga za Taifa (hekta 4.2 millioni), hifadhi za
wanyama (hekta 7.7 millioni) na hifadhi za misitu (hekta 10.1
millioni). Eneo lote
linalolimwa kwa mwaka ni kama hekta 5.1 millioni ambazo ni
asilimia 5 ya uso wa Tanzania.
Ardhi ile nyingine ifaayo kilimo, lakini haijalimwa, ni
hekta 10 milioni, na sehemu kubwa ikiwa inatumiwa kulisha mifugo.
Ndani ya hifadhi, kuna hekta nyingine milioni 4 zifaazo
kilimo.
Sheria ya Ardhi 1999, na sheria ya aridhi ya Vijiji
1999
Sheria
ya Ardhi na Sheria ya Ardhi ya Vijiji kwa pamoja ni sheria
zinazoweka misingi ya kutawala na kusimamia ardhi, kusuluhisha
migogoro na mengine yanayohusiana. Utekelezaji wa sheria hizi
utahitaji uelimishaji wa washika dau wote
kuhusu haki na wajibu
wao, ili waweze kushiriki kikamilifu katika kuitekeleza.
Wajibu wa Sekta za Umma/Binafsi
Wizara
zote, taasisi za umma na binafsi, ambazo shughuli zake zinahusiana
na maendeleo ya ardhi, yabidi zifanye kazi kwa pamoja na Waziri
anayesimamia masuala ya ardhi kuhakikisha kunakuweko ufanisi
katika utekelezaji wa Sera ya Ardhi. Aidha, Serikali za Mitaa
zinatakiwa zifanye kazi kwa pamoja na Waziri anayesimamia ardhi
ili uwepo usimamizi sahihi wa ardhi katika maeneo ya mamlaka zao.